Mwanzo 6:5-8
Mwanzo 6:5-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu alipoona wingi wa uovu wa binadamu duniani, na kwamba kila analokusudia binadamu moyoni mwake ni ovu daima, Mwenyezi-Mungu alisikitika sana kwa kumuumba binadamu duniani. Mwenyezi-Mungu alihuzunika sana moyoni mwake, hivyo akasema, “Nitamfuta kabisa duniani binadamu niliyemuumba; nitafutilia mbali pia wanyama wa porini, viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Ninasikitika kwamba niliwaumba duniani.” Lakini Noa alipata fadhili mbele ya Mwenyezi-Mungu.
Mwanzo 6:5-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote. BWANA akaghairi kwa kuwa amemwumba mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewaumba. Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.
Mwanzo 6:5-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.
Mwanzo 6:5-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA akaona jinsi uovu wa mwanadamu ulivyokuwa mkubwa duniani, na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu. BWANA akasikitika kwamba alimuumba mwanadamu duniani, na moyo wa Mungu ukasikitika sana. Kwa hiyo BWANA akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba kutoka uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na viumbe vinavyotambaa ardhini, na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika kuwaumba.” Lakini Nuhu akapata kibali machoni pa BWANA.