Mwanzo 6:5-6
Mwanzo 6:5-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu alipoona wingi wa uovu wa binadamu duniani, na kwamba kila analokusudia binadamu moyoni mwake ni ovu daima, Mwenyezi-Mungu alisikitika sana kwa kumuumba binadamu duniani. Mwenyezi-Mungu alihuzunika sana moyoni mwake
Mwanzo 6:5-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote. BWANA akaghairi kwa kuwa amemwumba mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.
Mwanzo 6:5-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.
Mwanzo 6:5-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA akaona jinsi uovu wa mwanadamu ulivyokuwa mkubwa duniani, na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu. BWANA akasikitika kwamba alimuumba mwanadamu duniani, na moyo wa Mungu ukasikitika sana.