Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 5:1-24

Mwanzo 5:1-24 Biblia Habari Njema (BHN)

Ifuatayo ni orodha ya wazawa wa Adamu. Wakati Mungu alipomuumba binadamu, alimuumba kwa mfano wake. Aliwaumba mwanamume na mwanamke, kisha akawabariki na kuwapa jina “Binadamu.” Adamu alipokuwa na umri wa miaka 130, alipata mtoto aliyefanana naye, na mwenye sura kama yake; akamwita Sethi. Baada ya kumzaa Sethi, Adamu aliishi miaka 800, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Adamu alifariki akiwa na umri wa miaka 930. Sethi alipokuwa na umri wa miaka 105, alimzaa Enoshi. Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Sethi alifariki akiwa na umri wa miaka 912. Enoshi alipokuwa na umri wa miaka 90, alimzaa Kenani. Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Enoshi alifariki akiwa na umri wa miaka 905. Kenani alipokuwa na umri wa miaka 70, alimzaa Mahalaleli. Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Kenani alifariki akiwa na umri wa miaka 910. Mahalaleli alipokuwa na umri wa miaka 65, alimzaa Yaredi. Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Mahalaleli alifariki akiwa na umri wa miaka 895. Yaredi alipokuwa na umri wa miaka 162, alimzaa Henoki. Baada ya kumzaa Henoki, Yaredi aliishi miaka 800 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Yaredi alifariki akiwa na umri wa miaka 962. Henoki alipokuwa na umri wa miaka 65, alimzaa Methusela. Henoki alikuwa mcha Mungu. Baada ya kumzaa Methusela, Henoki aliishi miaka 300 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Henoki aliishi miaka 365. Alikuwa mcha Mungu, akatoweka, kwa maana Mungu alimchukua.

Shirikisha
Soma Mwanzo 5

Mwanzo 5:1-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa. Adamu akaishi miaka mia moja na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi. Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia tisa na thelathini, naye akafa. Sethi akaishi miaka mia moja na mitano, akamzaa Enoshi. Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Sethi ni miaka mia tisa na kumi na miwili, akafa. Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani. Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Enoshi ni miaka mia tisa na mitano, akafa. Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arubaini, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Kenani ni miaka mia tisa na kumi, akafa. Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa. Yaredi akaishi miaka mia moja na sitini na miwili, akamzaa Henoko. Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Yaredi ni miaka mia tisa na sitini na miwili, akafa. Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. Henoko akaenda pamoja na Mungu. Baada ya kumzaa Methusela aliishi miaka mia tatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.

Shirikisha
Soma Mwanzo 5

Mwanzo 5:1-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa. Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi. Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa. Sethi akaishi miaka mia na mitano, akamzaa Enoshi. Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa. Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani. Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa. Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na kumi, akafa. Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa. Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko. Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa. Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.

Shirikisha
Soma Mwanzo 5

Mwanzo 5:1-24 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu. Mungu alipomuumba mwanadamu, alimfanya kwa sura ya Mungu. Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “Binadamu.” Adamu alipokuwa ameishi miaka mia moja na thelathini, alimzaa mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita jina Sethi. Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka mia nane, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Adamu aliishi jumla ya miaka mia tisa na thelathini, ndipo akafa. Sethi alipokuwa ameishi miaka mia moja na tano, akamzaa Enoshi. Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka mia nane na saba (807), akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Sethi aliishi jumla ya miaka mia tisa na kumi na mbili (912), ndipo akafa. Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani. Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka mia nane na kumi na tano (815), naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Enoshi aliishi jumla ya miaka mia tisa na tano (905), ndipo akafa. Kenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka mia nane na arobaini, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Kenani aliishi jumla ya miaka mia tisa na kumi, ndipo akafa. Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, akamzaa Yaredi. Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka mia nane na thelathini, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Mahalaleli aliishi jumla ya miaka mia nane tisini na tano (895), ndipo akafa. Yaredi alipokuwa ameishi miaka mia moja na sitini na mbili (162), akamzaa Henoko. Baada ya kumzaa Henoko, Yaredi aliishi miaka mia nane, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Yaredi aliishi jumla ya miaka mia tisa na sitini na mbili (962), ndipo akafa. Henoko alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, akamzaa Methusela. Baada ya kumzaa Methusela, Henoko alitembea na Mungu miaka mia tatu, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Henoko aliishi jumla ya miaka mia tatu sitini na tano (365). Henoko akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua.

Shirikisha
Soma Mwanzo 5