Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 49:3-27

Mwanzo 49:3-27 Biblia Habari Njema (BHN)

“Wewe Reubeni ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu yangu na tunda la ujana wangu. Wewe wawapita ndugu zako kwa ukuu na nguvu. “Wewe ni kama maji ya mafuriko. Lakini hutakuwa wa kwanza tena, maana ulipanda kitandani mwangu mimi baba yako, wewe ulikitia najisi; naam wewe ulikipanda! “Simeoni na Lawi ni ndugu: Silaha zao wanatumia kufanya ukatili, lakini mimi sitashiriki njama zao; ee roho yangu, usishiriki mikutano yao, maana, katika hasira yao, walimuua mtu, kwa utundu wao walikata mshipa wa ng'ombe. “Nalaani hasira yao maana ni kali mno, na ghadhabu yao isiyo na huruma. Nitawatawanya katika nchi ya Yakobo, nitawasambaza katika nchi ya Israeli. “Wewe Yuda, ndugu zako watakusifu. Adui zako utawakaba shingo; na ndugu zako watainama mbele yako. “Wewe Yuda, mwanangu, ni kama mwanasimba ambaye amepata mawindo yake akapanda juu. Kama simba hujinyosha na kulala chini; simba mwenye nguvu, nani athubutuye kumwamsha? “Fimbo ya kifalme haitatoka kwa Yuda, wala bakora ya utawala miguuni pake, mpaka atakapofika yule ambaye ni yake; ambaye mataifa yatamtii. “Atafunga punda wake katika mzabibu na mwanapunda wake kwenye mzabibu bora. Hufua nguo zake katika divai, na mavazi yake katika divai nyekundu. “Macho yake ni mekundu kwa divai, meno yake ni meupe kwa maziwa. “Zebuluni ataishi sehemu za pwani, pwani yake itakuwa mahali pa kuegesha meli. Nchi yake itapakana na Sidoni. “Isakari ni kama punda mwenye nguvu, ajilazaye kati ya mizigo yake. “Aliona kuwa mahali pa kupumzikia ni pema, na kwamba nchi ni ya kupendeza, akauinamisha mgongo wake kubeba mzigo, akawa mtumwa kufanya kazi za shuruti. “Dani atakuwa mwamuzi wa watu wake, kama mojawapo ya makabila ya Israeli. “Atakuwa kama nyoka njiani, nyoka mwenye sumu kando ya njia, aumaye visigino vya farasi, naye mpandafarasi huanguka chali. “Ee Mwenyezi-Mungu, nangojea uniokoe! “Gadi atashambuliwa na wanyanganyi, lakini yeye atawafuata nyuma na kuwashambulia. “Ardhi ya Asheri itatoa mavuno kwa wingi, naye atatoa chakula kimfaacho mfalme. “Naftali ni kama paa aliye huru, azaaye watoto walio wazuri. “Yosefu ni kama mti uzaao, mti uzaao kando ya chemchemi, matawi yake hutanda ukutani. “Wapiga mishale walimshambulia vikali, wakamtupia mishale na kumsumbua sana. “Lakini upinde wake bado imara, na mikono yake imepewa nguvu, kwa uwezo wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli; “kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia, kwa Mungu mwenye nguvu atakayekubariki; upate baraka za mvua toka juu mbinguni, baraka za maji ya vilindi vilivyo chini, baraka za uzazi wa akina mama na mifugo. Baraka za baba yako zishinde baraka za milima ya milele, ziwe bora kuliko vilima vya kale. Baraka hizo na ziwe juu ya kichwa cha Yosefu, juu ya paji lake yeye aliyekuwa ametengwa na ndugu zake. “Benyamini ni mbwamwitu mkali; asubuhi hula mawindo yake, na jioni hugawa nyara.”

Shirikisha
Soma Mwanzo 49

Mwanzo 49:3-27 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. Umekuwa kama maji yavukavyo mpaka, basi nawe hutafana tena, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu. Simeoni na Lawi ni ndugu; Panga zao ni silaha za jeuri. Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimwua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe; Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli. Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia. Yuda ni mwanasimba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemwamsha? Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwanapunda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu. Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa. Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni. Isakari ni punda hodari, Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo; Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu. Dani atahukumu watu wake, Kama moja ya makabila ya Israeli; Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Na apandaye akaanguka chali. Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA. Gadi, jeshi litamsonga, Lakini atawasonga wao mpaka visigino. Asheri, chakula chake kitakuwa kinono, Naye atatoa tunu za kifalme. Naftali ni ayala aliyefunguliwa; Anatoa maneno mazuri. Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matawi yake yametanda ukutani. Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamlenga na kumbana sana Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye mwamba wa Israeli, Naam, kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia; Kwa baraka za juu mbinguni. Baraka za vilindi vilivyo chini, Baraka za maziwa, na za mimba. Baraka za baba yako Ni nyingi kuliko za milima ya kale, Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake, yeye aliyeteuliwa kati ya ndugu zake. Benyamini ni mbwamwitu mwenye kuraruararua Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka.

Shirikisha
Soma Mwanzo 49

Mwanzo 49:3-27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu. Simeoni na Lawi ni ndugu; Panga zao ni silaha za jeuri. Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng’ombe; Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli. Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia. Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha? Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu. Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa. Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni. Isakari ni punda hodari, Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo; Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu. Dani atahukumu watu wake, Kama moja ya makabila ya Israeli; Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Hata apandaye ataanguka chali. Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA. Gadi, jeshi litamsonga, Lakini atawasonga wao mpaka visigino. Asheri, chakula chake kitakuwa kinono, Naye atatoa tunu za kifalme. Naftali ni ayala aliyefunguliwa; Anatoa maneno mazuri. Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matwi yake yametanda ukutani. Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamtupia, wakamwudhi, Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye jiwe la Israeli, Naam, kwa Mungu wa baba yako atakaye kusaidia; Kwa mibaraka ya mbinguni juu. Mibaraka ya vilindi vilivyo chini, Mibaraka ya maziwa, na ya mimba. Mibaraka ya baba yako Imepita mibaraka ya milima ya kale, Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliye mkuu kati ya ndugu zake. Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye kurarua-rarua Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka.

Shirikisha
Soma Mwanzo 49

Mwanzo 49:3-27 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

“Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu; umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo. Usiyezuiwa kama maji, basi hutakuwa mkuu tena, kwa kuwa ulipanda kwenye kitanda cha baba yako, kwenye kitanda changu na kukinajisi. “Simeoni na Lawi ni ndugu: panga zao ni silaha za jeuri. Mimi na nisiingie katika baraza lao, nami nisiunganike katika kusanyiko lao, kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao, na kukata mishipa ya miguu ya mafahali kama walivyopenda. Hasira yao na ilaaniwe, kwa kuwa ni kali mno, nayo ghadhabu yao ni ya ukatili! Nitawatawanya katika Yakobo, na kuwasambaza katika Israeli. “Yuda, ndugu zako watakusifu; mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako; wana wa baba yako watakusujudia. Ee Yuda, wewe ni mwana simba; unarudi toka mawindoni, mwanangu. Kama simba hunyemelea na kulala chini, kama simba jike: nani athubutuye kumwamsha? Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda, wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake, hadi aje yeye ambaye milki ni yake, ambaye utii wa mataifa ni wake. Atamfunga punda wake katika mzabibu, naye mwana-punda wake kwenye tawi lililo bora zaidi; atafua mavazi yake katika divai, majoho yake katika damu ya mizabibu. Macho yake yatakuwa mekundu kwa divai, meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa. “Zabuloni ataishi pwani ya bahari na kuwa bandari za kuegesha meli; mpaka wake utapanuka kuelekea Sidoni. “Isakari ni punda mwenye nguvu ambaye amelala kati ya mizigo yake. Aonapo palivyo pazuri mahali pake pa kupumzika na jinsi nchi yake inavyopendeza, atainamisha bega lake kwenye mzigo na kujitolea kwa ajili ya kazi ngumu. “Dani atahukumu watu wake kwa haki kama mmoja wa makabila ya Israeli. Dani atakuwa nyoka kando ya barabara, nyoka mwenye sumu kando ya njia, yule aumaye visigino vya farasi ili yule ampandaye aanguke chali. “Ee BWANA, nautafuta wokovu wako. “Gadi atashambuliwa ghafula na kundi la washambuliaji, lakini yeye atawageukia na kuwashinda kabisa. “Chakula cha Asheri kitakuwa kinono, naye atatoa chakula kitamu kinachomfaa mfalme. “Naftali ni kulungu jike aliyeachiwa huru azaaye watoto wazuri. “Yusufu ni mzabibu uzaao, mzabibu uzaao ulio kando ya chemchemi, ambao matawi yake hutanda ukutani. Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia, wakampiga mshale kwa ukatili. Lakini upinde wake ulibaki imara, mikono yake ikatiwa nguvu, na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli, kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, kwa sababu ya Mwenyezi, yeye anayekubariki kwa baraka za juu mbinguni, baraka za kilindi kilichoko chini, baraka za matitini na za tumbo la uzazi. Baraka za baba yako ni kubwa kuliko baraka za milima ya kale, nyingi kuliko vilima vya kale. Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yusufu, juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake. “Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye njaa kuu; asubuhi hurarua mawindo yake, jioni hugawa nyara.”

Shirikisha
Soma Mwanzo 49