Mwanzo 49:22-26
Mwanzo 49:22-26 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Yusufu ni mzabibu uzaao, mzabibu uzaao ulio kando ya chemchemi, ambao matawi yake hutanda ukutani. Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia, wakampiga mshale kwa ukatili. Lakini upinde wake ulibaki imara, mikono yake ikatiwa nguvu, na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli, kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, kwa sababu ya Mwenyezi, yeye anayekubariki kwa baraka za juu mbinguni, baraka za kilindi kilichoko chini, baraka za matitini na za tumbo la uzazi. Baraka za baba yako ni kubwa kuliko baraka za milima ya kale, nyingi kuliko vilima vya kale. Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yusufu, juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake.
Mwanzo 49:22-26 Biblia Habari Njema (BHN)
“Yosefu ni kama mti uzaao, mti uzaao kando ya chemchemi, matawi yake hutanda ukutani. “Wapiga mishale walimshambulia vikali, wakamtupia mishale na kumsumbua sana. “Lakini upinde wake bado imara, na mikono yake imepewa nguvu, kwa uwezo wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli; “kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia, kwa Mungu mwenye nguvu atakayekubariki; upate baraka za mvua toka juu mbinguni, baraka za maji ya vilindi vilivyo chini, baraka za uzazi wa akina mama na mifugo. Baraka za baba yako zishinde baraka za milima ya milele, ziwe bora kuliko vilima vya kale. Baraka hizo na ziwe juu ya kichwa cha Yosefu, juu ya paji lake yeye aliyekuwa ametengwa na ndugu zake.
Mwanzo 49:22-26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matawi yake yametanda ukutani. Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamlenga na kumbana sana Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye mwamba wa Israeli, Naam, kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia; Kwa baraka za juu mbinguni. Baraka za vilindi vilivyo chini, Baraka za maziwa, na za mimba. Baraka za baba yako Ni nyingi kuliko za milima ya kale, Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake, yeye aliyeteuliwa kati ya ndugu zake.
Mwanzo 49:22-26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matwi yake yametanda ukutani. Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamtupia, wakamwudhi, Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye jiwe la Israeli, Naam, kwa Mungu wa baba yako atakaye kusaidia; Kwa mibaraka ya mbinguni juu. Mibaraka ya vilindi vilivyo chini, Mibaraka ya maziwa, na ya mimba. Mibaraka ya baba yako Imepita mibaraka ya milima ya kale, Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliye mkuu kati ya ndugu zake.