Mwanzo 49:22-24
Mwanzo 49:22-24 Biblia Habari Njema (BHN)
“Yosefu ni kama mti uzaao, mti uzaao kando ya chemchemi, matawi yake hutanda ukutani. “Wapiga mishale walimshambulia vikali, wakamtupia mishale na kumsumbua sana. “Lakini upinde wake bado imara, na mikono yake imepewa nguvu, kwa uwezo wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli
Mwanzo 49:22-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matawi yake yametanda ukutani. Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamlenga na kumbana sana Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye mwamba wa Israeli
Mwanzo 49:22-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matwi yake yametanda ukutani. Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamtupia, wakamwudhi, Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye jiwe la Israeli
Mwanzo 49:22-24 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Yusufu ni mzabibu uzaao, mzabibu uzaao ulio kando ya chemchemi, ambao matawi yake hutanda ukutani. Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia, wakampiga mshale kwa ukatili. Lakini upinde wake ulibaki imara, mikono yake ikatiwa nguvu, na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli