Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 49:14-27

Mwanzo 49:14-27 Biblia Habari Njema (BHN)

“Isakari ni kama punda mwenye nguvu, ajilazaye kati ya mizigo yake. “Aliona kuwa mahali pa kupumzikia ni pema, na kwamba nchi ni ya kupendeza, akauinamisha mgongo wake kubeba mzigo, akawa mtumwa kufanya kazi za shuruti. “Dani atakuwa mwamuzi wa watu wake, kama mojawapo ya makabila ya Israeli. “Atakuwa kama nyoka njiani, nyoka mwenye sumu kando ya njia, aumaye visigino vya farasi, naye mpandafarasi huanguka chali. “Ee Mwenyezi-Mungu, nangojea uniokoe! “Gadi atashambuliwa na wanyanganyi, lakini yeye atawafuata nyuma na kuwashambulia. “Ardhi ya Asheri itatoa mavuno kwa wingi, naye atatoa chakula kimfaacho mfalme. “Naftali ni kama paa aliye huru, azaaye watoto walio wazuri. “Yosefu ni kama mti uzaao, mti uzaao kando ya chemchemi, matawi yake hutanda ukutani. “Wapiga mishale walimshambulia vikali, wakamtupia mishale na kumsumbua sana. “Lakini upinde wake bado imara, na mikono yake imepewa nguvu, kwa uwezo wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli; “kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia, kwa Mungu mwenye nguvu atakayekubariki; upate baraka za mvua toka juu mbinguni, baraka za maji ya vilindi vilivyo chini, baraka za uzazi wa akina mama na mifugo. Baraka za baba yako zishinde baraka za milima ya milele, ziwe bora kuliko vilima vya kale. Baraka hizo na ziwe juu ya kichwa cha Yosefu, juu ya paji lake yeye aliyekuwa ametengwa na ndugu zake. “Benyamini ni mbwamwitu mkali; asubuhi hula mawindo yake, na jioni hugawa nyara.”

Shirikisha
Soma Mwanzo 49

Mwanzo 49:14-27 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

“Isakari ni punda mwenye nguvu ambaye amelala kati ya mizigo yake. Aonapo palivyo pazuri mahali pake pa kupumzika na jinsi nchi yake inavyopendeza, atainamisha bega lake kwenye mzigo na kujitolea kwa ajili ya kazi ngumu. “Dani atahukumu watu wake kwa haki kama mmoja wa makabila ya Israeli. Dani atakuwa nyoka kando ya barabara, nyoka mwenye sumu kando ya njia, yule aumaye visigino vya farasi ili yule ampandaye aanguke chali. “Ee BWANA, nautafuta wokovu wako. “Gadi atashambuliwa ghafula na kundi la washambuliaji, lakini yeye atawageukia na kuwashinda kabisa. “Chakula cha Asheri kitakuwa kinono, naye atatoa chakula kitamu kinachomfaa mfalme. “Naftali ni kulungu jike aliyeachiwa huru azaaye watoto wazuri. “Yusufu ni mzabibu uzaao, mzabibu uzaao ulio kando ya chemchemi, ambao matawi yake hutanda ukutani. Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia, wakampiga mshale kwa ukatili. Lakini upinde wake ulibaki imara, mikono yake ikatiwa nguvu, na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli, kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, kwa sababu ya Mwenyezi, yeye anayekubariki kwa baraka za juu mbinguni, baraka za kilindi kilichoko chini, baraka za matitini na za tumbo la uzazi. Baraka za baba yako ni kubwa kuliko baraka za milima ya kale, nyingi kuliko vilima vya kale. Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yusufu, juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake. “Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye njaa kuu; asubuhi hurarua mawindo yake, jioni hugawa nyara.”

Shirikisha
Soma Mwanzo 49