Mwanzo 49:10-11
Mwanzo 49:10-11 Biblia Habari Njema (BHN)
“Fimbo ya kifalme haitatoka kwa Yuda, wala bakora ya utawala miguuni pake, mpaka atakapofika yule ambaye ni yake; ambaye mataifa yatamtii. “Atafunga punda wake katika mzabibu na mwanapunda wake kwenye mzabibu bora. Hufua nguo zake katika divai, na mavazi yake katika divai nyekundu.
Mwanzo 49:10-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwanapunda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.
Mwanzo 49:10-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.
Mwanzo 49:10-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda, wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake, hadi aje yeye ambaye milki ni yake, ambaye utii wa mataifa ni wake. Atamfunga punda wake katika mzabibu, naye mwana-punda wake kwenye tawi lililo bora zaidi; atafua mavazi yake katika divai, majoho yake katika damu ya mizabibu.