Mwanzo 40:1-4
Mwanzo 40:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Wakati fulani baada ya mambo hayo, maofisa wawili wa mfalme wa Misri walimkosea mfalme. Maofisa hao walikuwa mtunza vinywaji mkuu na mwoka mikate mkuu wa mfalme. Farao aliwakasirikia hao maofisa wake wawili, akawafungia ndani ya ngome ya mkuu wa kikosi cha ulinzi, katika gereza, mahali alipofungwa Yosefu. Mkuu wa kikosi cha ulinzi akamteua Yosefu awatumikie. Nao wakawa kifungoni kwa muda fulani.
Mwanzo 40:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikawa, baada ya mambo hayo, mnyweshaji wa mfalme wa Misri, na mwokaji wake, wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri. Farao akawaghadhibikia maofisa wake wawili, mkuu wa wanyweshaji na mkuu wa waokaji. Akawatia katika ulinzi nyumbani mwa mkuu wa askari, humo gerezani, mahali alipofungwa Yusufu. Mkuu wa askari akamwekea Yusufu watu hao, naye akawahudumia, nao wakakaa siku kadhaa katika kifungo.
Mwanzo 40:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa, baada ya mambo hayo, mnyweshaji wa mfalme wa Misri, na mwokaji wake, wakamkosa bwana wao, mfalme wa Misri. Farao akawaghadhibikia maakida wake wawili, mkuu wa wanyweshaji na mkuu wa waokaji. Akawatia katika lindo nyumbani mwa mkuu wa askari, humo gerezani, mahali alipofungwa Yusufu. Mkuu wa askari akamwekea Yusufu watu hao, naye akawahudumu, nao wakakaa siku kadha wa kadha katika kifungo.
Mwanzo 40:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baada ya muda, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri. Farao akawakasirikia hawa maafisa wake wawili, mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu. Akawaweka chini ya ulinzi katika nyumba ya mkuu wa walinzi, katika gereza lile lile alimofungwa Yusufu. Mkuu wa walinzi akawakabidhi kwa Yusufu, naye akawahudumia. Walipokuwa wamekaa chini ya ulinzi kwa muda