Mwanzo 37:3-4
Mwanzo 37:3-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko ndugu zake wote, kwa sababu alikuwa mwanawe wa uzeeni; akamshonea joho lililofumwa vizuri sana. Ndugu zake walipoona kwamba baba yao anampenda Yusufu kuliko yeyote kati yao, walimchukia na hawakusema naye neno lolote jema.
Mwanzo 37:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Israeli alimpenda Yosefu kuliko watoto wake wote kwa sababu alikuwa amezaliwa wakati wa uzee wake. Alimshonea Yosefu kanzu ndefu. Lakini ndugu zake walipoona kwamba baba yao alimpenda Yosefu kuliko wao, wakamchukia hata hawakuzungumza naye kwa amani.
Mwanzo 37:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee wake, akamfanyia kanzu ndefu. Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia, wala hawakuweza kusema naye kwa amani.
Mwanzo 37:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)