Mwanzo 37:10-11
Mwanzo 37:10-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini alipomsimulia baba yake na ndugu zake ndoto hiyo, baba yake alimkemea akisema, “Ni ndoto gani hiyo uliyoota? Je, itatulazimu mimi, mama yako na ndugu zako kuja kuinama chini kwa heshima mbele yako?” Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akawa analifikiria jambo hilo.
Mwanzo 37:10-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie mpaka chini? Ndugu zake wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili.
Mwanzo 37:10-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi? Ndugu zake wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili.
Mwanzo 37:10-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Alipomwambia baba yake pamoja na ndugu zake, baba yake akamkemea akisema, “Ni ndoto gani hii uliyoota? Hivi kweli mama yako, na mimi, na ndugu zako tutakuja kukusujudia wewe?” Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akaliweka jambo hilo moyoni.