Mwanzo 3:7-8
Mwanzo 3:7-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Mara macho yao yakafumbuliwa, wakatambua kwamba wako uchi; hivyo wakajishonea majani ya mtini, wakajifanyia mavazi ya kiunoni. Jioni, wakati wa kupunga upepo, huyo mwanamume na mkewe wakasikia hatua za Mwenyezi-Mungu akitembea bustanini, nao wakajificha kati ya miti ya bustani, Mwenyezi-Mungu asipate kuwaona.
Mwanzo 3:7-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajitambua kuwa wako uchi, wakashona majani ya mtini, na kujifanyia mavazi ya kusitiri uchi wao. Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.
Mwanzo 3:7-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo. Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.
Mwanzo 3:7-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika. Yule mwanaume na mkewe waliposikia sauti ya BWANA Mungu akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka kwa BWANA Mungu katikati ya miti ya bustani.