Mwanzo 3:1-2
Mwanzo 3:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini walioumbwa na Mwenyezi-Mungu. Basi, nyoka akamwambia huyo mwanamke, “Ati Mungu alisema msile matunda ya mti wowote bustanini?” Mwanamke akamjibu huyo nyoka, “Twaweza kula matunda ya mti wowote bustanini
Mwanzo 3:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula
Mwanzo 3:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula
Mwanzo 3:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Basi nyoka alikuwa mjanja kuliko wanyama pori wote ambao BWANA Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?” Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyo katika bustani