Mwanzo 27:28-29
Mwanzo 27:28-29 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu akumiminie umande wa mbinguni; akupe ardhi yenye rutuba, nafaka na divai kwa wingi. Jamii za watu zikutumikie, na mataifa yakuinamie kwa heshima. Uwe mtawala wa ndugu zako, watoto wa kiume wa mama yako wakuinamie kwa heshima. Kila akulaaniye na alaaniwe, kila akubarikiye na abarikiwe!”
Mwanzo 27:28-29 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo. Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Alaaniwe yeyote yule atakayekulaani, Na abarikiwe yeyote yule atakayekubariki.
Mwanzo 27:28-29 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo. Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe.
Mwanzo 27:28-29 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mungu na akupe umande wa mbinguni na utajiri wa duniani: wingi wa nafaka na divai mpya. Mataifa yakutumikie, na mataifa yakusujudie. Uwe bwana juu ya ndugu zako, na wana wa mama yako wakusujudie. Walaaniwe wale wanaokulaani, na wabarikiwe wale wanaokubariki.”