Mwanzo 21:1-3
Mwanzo 21:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu alimkumbuka Sara, akamtendea kama alivyoahidi. Basi, Abrahamu akiwa mzee, Sara akapata mimba, akamzalia mtoto wa kiume, wakati uleule Mungu alioutaja. Abrahamu akampa huyo mwanawe ambaye Sara alimzalia jina Isaka.
Mwanzo 21:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema. Sara akapata mimba akamzalia Abrahamu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu. Abrahamu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia.
Mwanzo 21:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema. Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu. Ibrahimu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia.
Mwanzo 21:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wakati huu BWANA akamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, na BWANA akamtendea Sara kama alivyoahidi. Sara akapata mimba, na akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, katika majira yale Mungu alikuwa amemwahidi. Abrahamu akampa huyo mwana ambaye Sara alimzalia jina Isaka.