Mwanzo 2:22-24
Mwanzo 2:22-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Na huo ubavu Mwenyezi-Mungu alioutoa kwa yule mwanamume akaufanya kuwa mwanamke, akamleta kwa huyo mwanamume. Ndipo huyo mwanamume akasema, “Naam! Huyu ni mfupa kutoka mifupa yangu, na nyama kutoka nyama yangu. Huyu ataitwa ‘Mwanamke’, kwa sababu ametolewa katika mwanamume.” Ndiyo maana mwanamume humwacha baba yake na mama yake, akaambatana na mkewe, nao wawili huwa mwili mmoja.
Mwanzo 2:22-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Mwanzo 2:22-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Mwanzo 2:22-24 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kisha BWANA Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwa ule ubavu alioutoa kwa mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa mwanaume. Huyo mwanaume akasema, “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu, na nyama ya nyama yangu, ataitwa ‘mwanamke’, kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.” Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.