Mwanzo 2:2-3
Mwanzo 2:2-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyofanya; siku hiyo ya saba Mungu akapumzika baada ya kazi yake yote aliyofanya. Mungu akaibariki siku ya saba na kuitakasa, kwa kuwa siku hiyo Mungu alipumzika baada ya kazi yake yote ya kuumba.
Mwanzo 2:2-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
Mwanzo 2:2-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
Mwanzo 2:2-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kufikia siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya; hivyo siku hiyo ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote. Mungu akaibariki siku ya saba, akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika baada ya kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya.