Mwanzo 2:16-17
Mwanzo 2:16-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Mwanzo 2:16-17 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wowote katika bustani; lakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.”
Mwanzo 2:16-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, “Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, Lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”
Mwanzo 2:16-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu alimwamuru huyo mwanamume, “Waweza kula matunda ya mti wowote katika bustani; lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usile, maana siku utakapokula matunda ya mti huo, hakika utakufa.”