Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 2:1-3 - Compare All Versions

Mwanzo 2:1-3 BHN (Biblia Habari Njema)

Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyokamilika pamoja na vitu vyote vilivyomo. Siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyofanya; siku hiyo ya saba Mungu akapumzika baada ya kazi yake yote aliyofanya. Mungu akaibariki siku ya saba na kuitakasa, kwa kuwa siku hiyo Mungu alipumzika baada ya kazi yake yote ya kuumba.

Shirikisha
Mwanzo 2 BHN

Mwanzo 2:1-3 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Basi mbingu na nchi zikamalizika kuumbwa, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.

Shirikisha
Mwanzo 2 SRUV

Mwanzo 2:1-3 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.

Shirikisha
Mwanzo 2 SUV

Mwanzo 2:1-3 NEN (Neno)

Kwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo. Kufikia siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya; hivyo siku hiyo ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote. Mungu akaibariki siku ya saba, akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika baada ya kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya.

Shirikisha
Mwanzo 2 NEN