Mwanzo 15:4-5
Mwanzo 15:4-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Ndipo Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Huyu hatakuwa mrithi wako! Mwanao halisi ndiye atakayekuwa mrithi wako.” Hapo Mwenyezi-Mungu akamleta Abramu nje na kumwambia, “Tazama mbinguni! Zihesabu nyota, kama kweli utaweza kuzihesabu! Hivyo ndivyo wazawa wako watakavyokuwa wengi!”
Mwanzo 15:4-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali utakayemzaa ndiye atakayekurithi. Akamtoa nje, akasema, Tazama juu mbinguni kisha uzihesabu nyota, kama unaweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
Mwanzo 15:4-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi. Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
Mwanzo 15:4-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo neno la BWANA lilipomjia, likanena: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi.” Akamtoa nje na kusema, “Tazama juu mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu.” Ndipo akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.”