Mwanzo 15:1-3
Mwanzo 15:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya mambo hayo, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Abramu katika maono, “Abramu! Usiogope! Mimi ni ngao yako. Tuzo lako litakuwa kubwa!” Lakini Abramu akasema, “Ee Mwenyezi-Mungu, utanipa nini hali naendelea kuishi bila mtoto, na mrithi wangu ni Eliezeri wa Damasko? Tazama! Hujanijalia mtoto; mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye atakayekuwa mrithi wangu!”
Mwanzo 15:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana. Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski? Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.
Mwanzo 15:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana. Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski? Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.
Mwanzo 15:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baada ya jambo hili, neno la BWANA likamjia Abramu katika maono, akaambiwa: “Usiogope, Abramu. Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.” Lakini Abramu akasema, “Ee BWANA Mwenyezi, utanipa nini na mimi sina mtoto, na atakayerithi nyumba yangu ni huyu Eliezeri Mdameski?” Abramu akasema, “Hukunipa watoto, hivyo mtumishi katika nyumba yangu ndiye atakuwa mrithi wangu.”