Mwanzo 13:14-17
Mwanzo 13:14-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya Loti kujitenga na Abramu, Mwenyezi-Mungu akamwambia Abramu, “Angalia toka hapo ulipo utazame pande zote: Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi. Nchi hii yote unayoiona nitakupa wewe na wazawa wako iwe yenu milele. Wazawa wako nitawafanya wawe wengi wasiohesabika, kama vile mavumbi ya nchi yasivyoweza kuhesabika! Basi, inuka uitembelee nchi hii katika mapana na marefu, kwani nitakupa wewe.”
Mwanzo 13:14-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi; maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele. Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi; ikiwa mtu ataweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, uzao wako nao utahesabika. Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo.
Mwanzo 13:14-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi; maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele. Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi; hata mtu akiweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, uzao wako nao utahesabika. Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo.
Mwanzo 13:14-17 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baada ya Lutu kuondoka, BWANA akamwambia Abramu, “Ukiwa hapo ulipo, inua macho yako utazame kaskazini na kusini, mashariki na magharibi. Nchi yote unayoiona nitakupa wewe na uzao wako hata milele. Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo ikiwa kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika. Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.”