Mwanzo 11:6-7
Mwanzo 11:6-7 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Mwenyezi Mungu akasema, “Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao. Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.”
Mwanzo 11:6-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu akasema, “Tazama, watu hawa ni taifa moja na wote wana lugha moja; huu ni mwanzo tu wa yale watakayoyafanya. Lolote wanalokusudia kulifanya watafanikiwa. Haya, na tushuke chini na kuivuruga lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.”
Mwanzo 11:6-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.
Mwanzo 11:6-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)