Mwanzo 10:1-7
Mwanzo 10:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya gharika, watoto wa Noa, Shemu, Hamu na Yafethi, walipata watoto wa kiume na wa kike. Hii ndiyo orodha ya wazawa wao: Watoto wa kiume wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. Watoto wa kiume wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Rifathi na Togama. Watoto wa kiume wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu na Dodanimu. Hawa ndio asili ya watu walioenea sehemu za pwani, kila watu kwa lugha yao, kwa jamaa zao na kufuata mataifa yao. Watoto wa kiume wa Hamu walikuwa Kushi, Misri, Puti na Kanaani. Watoto wa kiume wa Kushi walikuwa Seba, Hawila, Sabta, Raama na Sabteka. Watoto wa kiume wa Raama walikuwa Sheba na Dedani.
Mwanzo 10:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika. Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani. Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao. Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani.
Mwanzo 10:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika. Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani. Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao. Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani.
Mwanzo 10:1-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, yaani Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika. Wana wa Yafethi walikuwa: Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. Wana wa Gomeri walikuwa: Ashkenazi, Rifathi na Togarma. Wana wa Yavani walikuwa: Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. (Kutokana na hawa mataifa ya pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.) Wana wa Hamu walikuwa: Kushi, Misri, Putu na Kanaani. Wana wa Kushi walikuwa: Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa: Sheba na Dedani.