Mwanzo 10:1-32
Mwanzo 10:1-32 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya gharika, watoto wa Noa, Shemu, Hamu na Yafethi, walipata watoto wa kiume na wa kike. Hii ndiyo orodha ya wazawa wao: Watoto wa kiume wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. Watoto wa kiume wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Rifathi na Togama. Watoto wa kiume wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu na Dodanimu. Hawa ndio asili ya watu walioenea sehemu za pwani, kila watu kwa lugha yao, kwa jamaa zao na kufuata mataifa yao. Watoto wa kiume wa Hamu walikuwa Kushi, Misri, Puti na Kanaani. Watoto wa kiume wa Kushi walikuwa Seba, Hawila, Sabta, Raama na Sabteka. Watoto wa kiume wa Raama walikuwa Sheba na Dedani. Kushi alikuwa baba yake Nimrodi ambaye alikuwa shujaa wa kwanza duniani. Alikuwa mwindaji shujaa mbele ya Mwenyezi-Mungu, ndiyo maana kuna msemo usemao, “Kama Nimrodi mwindaji shujaa mbele ya Mwenyezi-Mungu.” Miji ya kwanza ya utawala wake ilikuwa Babuloni, Ereki na Akadi, katika nchi ya Shinari. Kutoka huko, Nimrodi alikwenda Ashuru, akajenga miji ya Ninewi, Rehoboth-iri, Kala na Reseni ulioko kati ya Ninewi na mji mkubwa wa Kala. Misri alikuwa babu wa Waludi, Waanamu, Walehabi, Wanaftuhi, Wapathrusi, Wakasluhi (ambao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori. Kanaani alikuwa babu yake Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, na pia babu yao Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, Wahivi, Waarki, Wasini, Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Baadaye watu wa jamii mbalimbali za Kanaani walitawanyika, hata eneo la nchi yao likawa toka Sidoni kuelekea kusini, hadi Gerari mpaka Gaza, na kuelekea mashariki hadi Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu hadi Lasha. Hao ndio wazawa wa Hamu kadiri ya makabila yao, lugha zao, nchi zao na mataifa yao. Shemu, mkubwa wa Yafethi, alikuwa baba yao Waebrania wote. Watoto wa kiume wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu. Watoto wa kiume wa Aramu walikuwa Usi, Huli, Getheri na Mashi. Arfaksadi alimzaa Shela, Shela akamzaa Eberi. Eberi alikuwa na watoto wa kiume wawili; wa kwanza akamwita Pelegi kwa sababu wakati huo watu duniani waligawanyika, na wa pili akamwita Yoktani. Yoktani alikuwa baba wa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, Hadoramu, Uzali, Dikla, Obali, Abimaeli, Sheba, Ofiri, Hawila na Yobabu. Hao wote walikuwa watoto wa Yoktani. Nchi walimokaa ilienea toka Mesha mpaka Sefari katika nyanda za juu za mashariki. Hao ndio wazawa wa Shemu, kadiri ya makabila yao, lugha zao, nchi zao na mataifa yao. Hao ndio jamaa za watoto wa Noa, kadiri ya vizazi vyao na mataifa yao. Kutokana nao mataifa yote yalienea duniani baada ya gharika.
Mwanzo 10:1-32 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika. Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani. Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao. Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani. Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za BWANA. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za BWANA. Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari. Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala; na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa. Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi, na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori. Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi, na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi, na Mhivi, na Mwarki, na Msini, na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyikana. Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha. Hao ndio wana wa Hamu, kufuata jamaa zao, kwa lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao. Naye Shemu ambaye ni baba wa wana wote wa Eberi, na ndugu mkubwa wa Yafethi, akazaliwa wana. Wana wa Shemu ni Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu. Na wana wa Aramu ni Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. Arfaksadi akamzaa Sela, Sela akamzaa Eberi. Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza ni Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye ni Yoktani. Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera, na Hadoramu, na Uzali, na Dikla, na Obali, na Abimaeli, na Seba, na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani. Makao yao yalikuwa kutoka Mesha kwa njia ya Sefari, mlima wa mashariki. Hao ndio wana wa Shemu, kufuata jamaa zao, na lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao. Hizo ndizo jamaa za wana wa Nuhu, kufuata vizazi vyao, katika mataifa yao; na kwa hao mataifa yaligawanyika katika nchi baada ya gharika.
Mwanzo 10:1-32 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika. Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani. Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao. Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani. Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za BWANA. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za BWANA. Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari. Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala; na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa. Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi, na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori. Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi, na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi, na Mhivi, na Mwarki, na Msini, na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyikana. Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha. Hao ndio wana wa Hamu, kufuata jamaa zao, kwa lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao. Naye Shemu ambaye ni baba wa wana wote wa Eberi, na ndugu mkubwa wa Yafethi, akazaliwa wana. Wana wa Shemu ni Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu. Na wana wa Aramu ni Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. Arfaksadi akamzaa Sela, Sela akamzaa Eberi. Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza ni Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye ni Yoktani. Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera, na Hadoramu, na Uzali, na Dikla, na Obali, na Abimaeli, na Seba, na Ofiri, na Havila, na Yobabi. Hao wote ndio wana wa Yoktani. Makao yao yalikuwa kutoka Mesha kwa njia ya Sefari, mlima wa mashariki. Hao ndio wana wa Shemu, kufuata jamaa zao, na lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao. Hizo ndizo jamaa za wana wa Nuhu, kufuata vizazi vyao, katika mataifa yao; na kwa hao mataifa yaligawanyika katika nchi baada ya gharika.
Mwanzo 10:1-32 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, yaani Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika. Wana wa Yafethi walikuwa: Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. Wana wa Gomeri walikuwa: Ashkenazi, Rifathi na Togarma. Wana wa Yavani walikuwa: Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. (Kutokana na hawa mataifa ya pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.) Wana wa Hamu walikuwa: Kushi, Misri, Putu na Kanaani. Wana wa Kushi walikuwa: Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa: Sheba na Dedani. Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa shujaa mwenye nguvu duniani. Alikuwa mwindaji hodari mbele za BWANA; Ndiyo maana watu husema, “Kama Nimrodi, mwindaji hodari mbele za BWANA.” Vituo vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne, katika nchi ya Shinari. Kutoka nchi ile alienda Ashuru, ambako alijenga miji ya Ninawi, na Rehoboth-Iri, na Kala, na Reseni, mji ulio kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa. Misri alikuwa baba wa: Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori. Kanaani alikuwa baba wa: Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi, Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, Wahivi, Waarki, Wasini, Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. (Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika, na mipaka ya Kanaani ikaenea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.) Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao. Shemu, ndugu mkubwa wa Yafethi, alizaa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi. Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu. Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mashi. Arfaksadi alikuwa baba wa Shela, naye Shela akamzaa Eberi. Eberi akapata wana wawili: Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani. Yoktani alikuwa baba wa: Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, Hadoramu, Uzali, Dikla, Obali, Abimaeli, Seba, Ofiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani. (Eneo waliloishi lilienea kutoka Mesha kuelekea Sefari, kwenye nchi ya vilima iliyo mashariki.) Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao. Hizi ndizo koo za wana wa Nuhu, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.