Wagalatia 6:4-6
Wagalatia 6:4-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini kila mmoja na aupime vizuri mwenendo wake mwenyewe. Ukiwa mwema, basi, anaweza kuona fahari juu ya alichofanya bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine. Maana kila mmoja anapaswa kuubeba mzigo wake mwenyewe. Mwenye kufundishwa neno la Mungu na amshirikishe mwalimu wake riziki zake.
Wagalatia 6:4-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. Maana kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe. Mwanafunzi na amshirikishe mwalimu wake katika mema yote.
Wagalatia 6:4-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe. Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote.
Wagalatia 6:4-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo aweze kujisifu, bila kujilinganisha na mtu mwingine. Kwa maana, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe. Basi, yeye afundishwaye katika neno na amshirikishe mwalimu wake mema yote.