Wagalatia 1:21-24
Wagalatia 1:21-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Baadaye nilikwenda katika tarafa za Siria na Kilikia. Wakati huo, mimi binafsi sikujulikana kwa jumuiya za Wakristo kule Yudea. Walichokuwa wanajua ni kile tu walichosikia: “Mtu yule aliyekuwa akitutesa hapo awali, sasa anaihubiri imani ileile aliyokuwa anajaribu kuiangamiza.” Basi, wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.
Wagalatia 1:21-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Baadaye nilikwenda pande za Shamu na Kilikia. Lakini sikujulikana uso wangu na makanisa ya Yudea yaliyokuwa katika Kristo; ila wamesikia tu ya kwamba huyo aliyetutesa hapo kwanza, sasa anaihubiri imani ile aliyoiharibu zamani. Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.
Wagalatia 1:21-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Baadaye nalikwenda pande za Shamu na Kilikia. Lakini sikujulikana uso wangu na makanisa ya Uyahudi yaliyokuwa katika Kristo; ila wamesikia tu ya kwamba huyo aliyetuudhi hapo kwanza, sasa anaihubiri imani ile aliyoiharibu zamani. Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.
Wagalatia 1:21-24 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baadaye nilienda sehemu za Siria na Kilikia. Lakini mimi binafsi sikujulikana kwa makanisa ya huko Yudea yaliyo katika Kristo. Wao walisikia habari tu kwamba, “Mtu yule ambaye hapo awali alikuwa akitutesa sasa anahubiri imani ile ile aliyokuwa akijaribu kuiangamiza.” Nao wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.