Ezra 7:9-10
Ezra 7:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu aliifanikisha sana safari yao waliyokuwa wameianza siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza. Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza sheria ya Mwenyezi-Mungu, kuitii na kuwafundisha watu wa Israeli maagizo na amri zake.
Ezra 7:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana alianza kukwea kutoka Babeli siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, naye akafika Yerusalemu siku ya kwanza ya mwezi wa tano, kama mkono mwema wa Mungu wake ulivyokuwa pamoja naye. Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya BWANA, na kuitenda, na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli.
Ezra 7:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana alianza kukwea kutoka Babeli siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, naye akafika Yerusalemu siku ya kwanza ya mwezi wa tano, kama mkono mwema wa Mungu wake ulivyokuwa pamoja naye. Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya BWANA, na kuitenda, na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli.
Ezra 7:9-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ezra alianza safari yake kutoka Babeli siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, naye akawasili Yerusalemu siku ya kwanza ya mwezi wa tano, kwa kuwa mkono wa neema wa Mungu wake ulikuwa juu yake. Kwa maana Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza na kushika sheria ya BWANA na kuwafundisha Waisraeli amri na sheria zake.