Ezekieli 6:9
Ezekieli 6:9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo katika mataifa walikochukuliwa mateka, watakaonusurika watanikumbuka. Watakumbuka jinsi nilivyohuzunishwa na mioyo yao ya uzinzi ambayo imegeuka kuwa mbali nami, na kwa macho yao ambayo yametamani sanamu zao. Watajichukia wenyewe kwa sababu ya uovu walioutenda na desturi zao za kuchukiza.
Ezekieli 6:9 Biblia Habari Njema (BHN)
Ndipo watakaponikumbuka mimi miongoni mwa hao watu wa mataifa ambamo watatawanyika. Watakumbuka jinsi nilivyowapiga kwa sababu mioyo yao isiyo na uaminifu ilinigeuka na kwa vile waliacha kunitazamia mimi wakazitazamia sanamu za miungu. Kwa hiyo watajichukia wao wenyewe kwa sababu ya maovu na machukizo yao yote waliyoyatenda.
Ezekieli 6:9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na hao wa kwenu watakaookoka watanikumbuka kati ya mataifa, watakakochukuliwa mateka, jinsi nilivyoiponda mioyo yao ya kikahaba, iliyoniacha, na macho yao, yaendayo kufanya uasherati na vinyago vyao; nao watajichukia nafsi zao machoni pao wenyewe, kwa sababu ya mabaya yao yote, waliyoyatenda kwa machukizo yao yote.
Ezekieli 6:9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)