Ezekieli 44:2-3
Ezekieli 44:2-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Lango hili litaendelea kufungwa. Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kulitumia, kwa sababu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimeingia kupitia lango hilo. Hivyo litadumu likiwa limefungwa. Hata hivyo, mkuu anayetawala anaweza kwenda huko na kula chakula chake kitakatifu mbele yangu. Ni lazima aingie na kutokea lango la chumba cha kuingilia.”
Ezekieli 44:2-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akaniambia, Lango hili litafungwa, halitafunguliwa, wala mtu awaye yote hataingia kwa lango hili, kwa maana BWANA, Mungu wa Israeli, ameingia kwa hilo; basi kwa sababu hiyo litafungwa. Na mkuu, yeye ndiye atakayeketi ndani yake ale chakula mbele za BWANA; ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango, naye atatoka kwa njia iyo hiyo.
Ezekieli 44:2-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akaniambia, Lango hili litafungwa, halitafunguliwa, wala mtu awaye yote hataingia kwa lango hili, kwa maana BWANA, Mungu wa Israeli, ameingia kwa hilo; basi kwa sababu hiyo litafungwa. Na mkuu, yeye ndiye atakayeketi ndani yake ale chakula mbele za BWANA; ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango, naye atatoka kwa njia iyo hiyo.
Ezekieli 44:2-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA akaniambia, “Lango hili litabaki limefungwa. Haliruhusiwi kufunguliwa, wala hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuingilia kwenye lango hili. Litabaki limefungwa kwa sababu BWANA, Mungu wa Israeli, ameingia kupitia lango hili. Yeye aliye mkuu peke yake ndiye anayeweza kukaa penye njia ya hilo lango na kula chakula mbele za BWANA. Itampasa aingie kwa njia hiyo ya lango la ukumbini na kutokea njia hiyo hiyo.”