Ezekieli 44:1-2
Ezekieli 44:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Yule mtu akanirudisha kwenye lango la nje linaloelekea mashariki, nje ya patakatifu, nalo lilikuwa limefungwa. Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Lango hili litaendelea kufungwa. Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kulitumia, kwa sababu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimeingia kupitia lango hilo. Hivyo litadumu likiwa limefungwa.
Ezekieli 44:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha akanirudisha kwa njia ya lango lile la nje, la mahali patakatifu lililoelekea upande wa mashariki; nalo lilikuwa limefungwa. BWANA akaniambia, Lango hili litafungwa, halitafunguliwa, wala mtu awaye yote hataingia kwa lango hili, kwa maana BWANA, Mungu wa Israeli, ameingia kwa hilo; basi kwa sababu hiyo litafungwa.
Ezekieli 44:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha akanirudisha kwa njia ya lango lile la nje, la mahali patakatifu lililoelekea upande wa mashariki; nalo lilikuwa limefungwa. BWANA akaniambia, Lango hili litafungwa, halitafunguliwa, wala mtu awaye yote hataingia kwa lango hili, kwa maana BWANA, Mungu wa Israeli, ameingia kwa hilo; basi kwa sababu hiyo litafungwa.
Ezekieli 44:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo yule mtu akanirudisha mpaka kwenye lango la nje la mahali patakatifu, lile linaloelekea upande wa mashariki, nalo lilikuwa limefungwa. BWANA akaniambia, “Lango hili litabaki limefungwa. Haliruhusiwi kufunguliwa, wala hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuingilia kwenye lango hili. Litabaki limefungwa kwa sababu BWANA, Mungu wa Israeli, ameingia kupitia lango hili.