Ezekieli 37:5-6
Ezekieli 37:5-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Bwana Mwenyezi-Mungu awaambia hivi: Nitaifanya pumzi iwaingie, nanyi mtaishi. Nitawatia mishipa na nyama, nitawafunika ngozi na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. Hapo mtajua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
Ezekieli 37:5-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Ezekieli 37:5-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Ezekieli 37:5-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hili ndilo asemalo BWANA Mwenyezi kwa hii mifupa: Nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. Nitawawekea mishipa, nami nitaifanya nyama ije juu yenu na kuwafunika kwa ngozi. Nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtakuwa hai. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi BWANA.’ ”