Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 3:7-9 - Compare All Versions

Ezekieli 3:7-9 BHN (Biblia Habari Njema)

Lakini Waisraeli hawatakusikiliza, kwani hawana nia ya kunisikiliza mimi. Watu wote wa Israeli ni wenye kichwa kigumu na moyo mkaidi. Nimekufanya uwe mgumu dhidi yao, na kichwa chako kitakuwa kigumu dhidi ya vichwa vyao vigumu. Kama almasi ilivyo ngumu kuliko jiwe gumu, ndivyo nilivyokufanya uwe kichwa kigumu. Usiwaogope wala usitishwe na nyuso zao, kwani hao ni watu waasi.”

Shirikisha
Ezekieli 3 BHN

Ezekieli 3:7-9 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Bali nyumba ya Israeli hawatakusikiliza wewe; kwa kuwa hawanisikilizi mimi; maana nyumba yote ya Israeli wana vipaji vigumu, na mioyo yenye ukaidi. Tazama, nimeufanya uso wako kuwa mgumu juu ya nyuso zao, na kipaji cha uso chako kuwa kigumu juu ya vipaji vya nyuso vyao. Kama almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyokifanya kipaji chako; usiwaogope, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba ya kuasi.

Shirikisha
Ezekieli 3 SUV

Ezekieli 3:7-9 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Bali nyumba ya Israeli hawatakusikiliza wewe; kwa kuwa hawanisikilizi mimi; maana nyumba yote ya Israeli wana vipaji vigumu, na mioyo yenye ukaidi. Tazama, nimeufanya uso wako kuwa mgumu juu ya nyuso zao, na kipaji cha uso chako kuwa kigumu juu ya vipaji vya nyuso zao. Kama almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyokifanya kipaji chako; usiwaogope, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba ya kuasi.

Shirikisha
Ezekieli 3 SRUV

Ezekieli 3:7-9 NEN (Neno)

Lakini nyumba ya Israeli haitakusikiliza, kwa kuwa hawako radhi kunisikiliza mimi, kwa kuwa nyumba yote ya Israeli ni wenye paji gumu na mioyo ya ukaidi. Tazama, nimefanya uso wako mgumu dhidi ya nyuso zao, na paji la uso wako gumu dhidi ya paji za nyuso zao. Kama vile almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyolifanya paji la uso wako. Usiwaogope wala usiwahofu, ijapokuwa ni nyumba ya uasi.”

Shirikisha
Ezekieli 3 NEN