Ezekieli 20:45-49
Ezekieli 20:45-49 Biblia Habari Njema (BHN)
Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia: “Wewe mtu, geukia upande wa kusini uhubiri dhidi ya nchi ya kusini, dhidi ya wakazi wa msitu wa Negebu. Waambie wasikilize neno langu mimi Mwenyezi-Mungu. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Nitawasha moto kwako, nao utateketeza miti yote, mibichi na mikavu; utaenea tangu kusini mpaka kaskazini wala hakuna atakayeweza kuzima miali yake. Kila mtu atausikia mchomo wake. Watu wote watajua kwamba ni mimi Mwenyezi-Mungu niliyeuwasha na hautazimika.” Kisha nami nikasema, “Ee Bwana Mwenyezi-Mungu! Watu wanalalamika juu yangu na kusema: ‘Huyu akisema, ni mafumbo tu!’”
Ezekieli 20:45-49 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Neno la BWANA likanijia, kusema, Mwanadamu, uelekeze uso wako kusini, ukadondoze neno lako upande wa kusini, ukatabiri juu ya msitu wa uwanda wa Negebu, ukauambie msitu wa Negebu, Lisikie neno la BWANA; Bwana MUNGU asema hivi; Tazama nitawasha moto ndani yako, nao utakula kila mti mbichi ndani yako, na kila mti mkavu; miali ya moto ule haitazimika, na nyuso zote toka kusini hadi kaskazini zitateketezwa kwa moto huo. Na watu wote wenye mwili wataona ya kuwa mimi, BWANA, nimeuwasha; hautazimika. Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, wao hunisema; Je! Mtu huyu si mtu mwenye kupiga mithali?
Ezekieli 20:45-49 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Neno la BWANA likanijia, kusema, Mwanadamu, uelekeze uso wako kusini, ukadondoze neno lako upande wa kusini, ukatabiri juu ya msitu wa uwanda wa Negebu, ukauambie msitu wa Negebu, Lisikie neno la BWANA; Bwana MUNGU asema hivi; Tazama nitawasha moto ndani yako, nao utakula kila mti mbichi ndani yako, na kila mti mkavu; miali ya moto ule haitazimika, na nyuso zote toka kusini hata kaskazini zitateketezwa kwa moto huo. Na watu wote wenye mwili wataona ya kuwa mimi, BWANA, nimeuwasha; hautazimika. Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, wao hunisema; Je! Mtu huyu si mtu mwenye kupiga mithali?
Ezekieli 20:45-49 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Neno la BWANA likanijia kusema: “Mwanadamu, uelekeze uso wako upande wa kusini, hubiri dhidi ya upande wa kusini, na utoe unabii dhidi ya msitu wa Negebu. Waambie watu wa Negebu: ‘Sikieni neno la BWANA. Hili ndilo asemalo BWANA Mwenyezi: Ninakaribia kukuwasha moto, nao utateketeza miti yako yote, mibichi na iliyokauka. Miali ya moto haitaweza kuzimwa na kila uso kutoka kusini mpaka kaskazini utakaushwa kwa moto huo. Kila mmoja ataona kuwa Mimi BWANA ndiye niliyeuwasha huo moto; nao hautazimwa.’ ” Ndipo niliposema, “Aa, BWANA Mwenyezi! Wao hunisema, ‘Huyu si huzungumza mafumbo tu?’ ”