Ezekieli 16:1-4
Ezekieli 16:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia: “Wewe mtu, ujulishe mji wa Yerusalemu machukizo yake. Uuambie kuwa, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nauambia Yerusalemu: Kwa asili wewe ulizaliwa katika nchi ya Kanaani. Baba yako alikuwa Mwamori, na mama yako alikuwa Mhiti. Siku ile ulipozaliwa, kitovu chako hakikukatwa wala hukuoshwa kwa maji; hukusuguliwa kwa chumvi wala hukuvishwa nguo za kitoto.
Ezekieli 16:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Neno la BWANA likanijia tena, kusema, Mwanadamu, uujulishe Yerusalemu machukizo yake, useme, Bwana MUNGU auambia Yerusalemu hivi; Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti. Na kuhusu habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa.
Ezekieli 16:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Neno la BWANA likanijia tena, kusema, Mwanadamu, uujulishe Yerusalemu machukizo yake, useme, Bwana MUNGU auambia Yerusalemu hivi; Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti. Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa.
Ezekieli 16:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Neno la BWANA likanijia kusema: “Mwanadamu, kabili Yerusalemu kuhusu matendo yake ya kuchukiza, useme, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi, analomwambia Yerusalemu: Asili na kuzaliwa kwako kulikuwa ni katika nchi ya Wakanaani; baba yako alikuwa Mwamori, naye mama yako alikuwa Mhiti. Siku uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuogeshwa kwa maji ili kukufanya safi, wala hukusuguliwa kwa chumvi wala kufunikwa kwa nguo.