Ezekieli 11:19-20
Ezekieli 11:19-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Nitawapeni moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu. Nitauondoa ule moyo mgumu kama jiwe na kuwapa moyo wa utii, ili mpate kufuata kanuni zangu na kuyatii maagizo yangu; nanyi mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu.
Ezekieli 11:19-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama; ili waende katika amri zangu, na kuyashika maagizo yangu, na kuyatenda; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
Ezekieli 11:19-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama; ili waende katika amri zangu, na kuyashika maagizo yangu, na kuyatenda; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
Ezekieli 11:19-20 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nitawapa moyo usiogawanyika na kuweka roho mpya ndani yao; nitaondoa ndani yao moyo wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama. Kisha watafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii sheria zangu. Watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao.