Kutoka 5:22-23
Kutoka 5:22-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Mose akamgeukia tena Mwenyezi-Mungu, akasema, “Ee Mwenyezi-Mungu, kwa nini unawatendea watu hawa uovu? Kwa nini hata ulinituma? Tangu nilipokwenda na kuongea na Farao kwa jina lako, yeye amewatendea uovu watu hawa. Wewe hujafanya lolote kuwakomboa watu wako.”
Kutoka 5:22-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Musa akarudi kwa BWANA, akasema, BWANA, mbona umewatenda mabaya watu hawa? Kwani kunituma mimi? Kwa maana tangu nilipokwenda kwa Farao, kusema naye kwa jina lako, amewatenda mabaya watu hawa; wala hukuwaokoa watu wako hata kidogo.
Kutoka 5:22-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Musa akarudi kwa BWANA, akasema, BWANA, mbona umewatenda mabaya watu hawa? Kwani kunituma mimi? Kwa maana tangu nilipokwenda kwa Farao, kusema naye kwa jina lako, amewatenda mabaya watu hawa; wala hukuwaokoa watu wako hata kidogo.
Kutoka 5:22-23 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Musa akarudi kwa BWANA na kumwambia, “Ee Bwana, mbona umewaletea watu hawa taabu? Kwa nini basi ukanituma mimi? Tangu nilipokwenda kuzungumza na Farao kwa jina lako, amewaletea watu hawa taabu, nawe kamwe hujawakomboa watu wako.”