Kutoka 5:1-2
Kutoka 5:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Baadaye, Mose na Aroni walimwendea Farao, wakamwambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli anasema hivi, ‘Waache watu wangu waondoke, wakanifanyie sikukuu jangwani.’” Lakini Farao akawauliza, “Ni nani huyo Mwenyezi-Mungu, hata nimsikilize na kuwaacha Waisraeli waondoke? Mimi simtambui huyo Mwenyezi-Mungu, wala sitawaruhusu Waisraeli waondoke.”
Kutoka 5:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hata baadaye, Musa na Haruni wakaenda wakamwambia Farao, wakasema, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Wape watu wangu ruhusa waende, ili kunifanyia sikukuu jangwani. Farao akasema, BWANA ni nani, hata niisikilize sauti yake, na kuwapa Israeli ruhusa waende zao? Mimi simjui BWANA, wala sitawapa Israeli ruhusa waende zao.
Kutoka 5:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hata baadaye, Musa na Haruni wakaenda wakamwambia Farao, wakasema, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Wape watu wangu ruhusa waende, ili kunifanyia sikukuu jangwani. Farao akasema, BWANA ni nani, hata niisikilize sauti yake, na kuwapa Israeli ruhusa waende zao? Mimi simjui BWANA, wala sitawapa Israeli ruhusa waende zao.
Kutoka 5:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baadaye Musa na Haruni wakaenda kwa Farao, wakamwambia, “Hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa Israeli: ‘Waruhusu watu wangu waende, ili waweze kunifanyia sikukuu huko jangwani.’ ” Farao akasema, “Huyo BWANA ni nani, hata nimtii na kuruhusu Waisraeli waende? Simjui huyo BWANA wala sitawaruhusu Waisraeli waende.”