Kutoka 4:14
Kutoka 4:14 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo hasira ya BWANA ikawaka dhidi ya Musa, akamwambia, “Vipi kuhusu ndugu yako, Haruni Mlawi? Ninajua yeye anaweza kuzungumza vizuri. Naye yuko tayari njiani kukulaki, na moyo wake utafurahi wakati atakapokuona.
Shirikisha
Soma Kutoka 4Kutoka 4:14 Biblia Habari Njema (BHN)
Ndipo hasira ya Mungu ilipowaka dhidi ya Mose, akamwambia, “Je, si yuko ndugu yako Aroni ambaye ni Mlawi? Najua yeye ana ufasaha wa kuongea. Tena anakuja kukutana nawe, na mara tu atakapokuona atafurahi moyoni.
Shirikisha
Soma Kutoka 4Kutoka 4:14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Musa, akasema, Je! Hayuko Haruni, ndugu yako, Mlawi? Najua ya kuwa yeye aweza kusema vizuri. Pamoja na hayo, tazama, anakuja kukulaki; naye atakapokuona, atafurahi moyoni mwake.
Shirikisha
Soma Kutoka 4