Kutoka 25:21-22
Kutoka 25:21-22 Biblia Habari Njema (BHN)
Ndani ya sanduku utaweka vibao viwili vya mawe na kukiweka kiti cha rehema juu yake. Mimi nitakutana nawe hapo; na kutoka juu ya kiti hicho cha rehema katikati ya viumbe hao walioko juu ya sanduku la ushuhuda, nitazungumza nawe na kukupa amri zote kwa ajili ya Waisraeli.
Kutoka 25:21-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.
Kutoka 25:21-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.
Kutoka 25:21-22 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Weka huo Ushuhuda nitakaokupa ndani ya hilo Sanduku la Agano, na uweke hicho kifuniko juu ya hilo Sanduku. Hapo juu ya hicho kifuniko, kati ya hao makerubi wawili walio juu ya hilo Sanduku la Ushuhuda, hapo ndipo nitakutana nawe na kukupa maagizo yangu kwa ajili ya Waisraeli.