Kutoka 20:13-17
Kutoka 20:13-17 Biblia Habari Njema (BHN)
“Usiue. “Usizini. “Usiibe. “Usimshuhudie jirani yako uongo. “Usiitamani nyumba ya jirani yako, wala mke wake, wala mtumwa wake wa kiume au wa kike, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala chochote kilicho mali ya jirani yako.”
Kutoka 20:13-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Usiue. Usizini. Usiibe. Usimshuhudie jirani yako uongo. Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako.
Kutoka 20:13-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Usiue. Usizini. Usiibe. Usimshuhudie jirani yako uongo. Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.
Kutoka 20:13-17 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Usiue. Usizini. Usiibe. Usimshuhudie jirani yako uongo. Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ngʼombe wake au punda wake, wala chochote kile alicho nacho jirani yako.”