Kutoka 17:1-3
Kutoka 17:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Kutoka jangwa la Sini, jumuiya yote ya Waisraeli ilisafiri hatua kwa hatua kama alivyoamuru Mwenyezi-Mungu, watu wakapiga kambi huko Refidimu. Lakini huko hakukuwa na maji ya kunywa. Kwa hiyo watu wakamnungunikia Mose wakisema, “Tupe maji ya kunywa.” Mose akawauliza, “Mbona mnaninungunikia? Mbona mnamjaribu Mwenyezi-Mungu?” Lakini wote walikuwa na kiu, wakamnungunikia Mose wakisema, “Kwa nini ulitutoa kule Misri utuue kwa kiu sisi sote na watoto wetu na mifugo yetu?”
Kutoka 17:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama BWANA alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe. Kwa hiyo hao watu wakamgombeza Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwa nini mnanigombeza? Mbona mnamjaribu BWANA? Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung'unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu?
Kutoka 17:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama BWANA alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe. Kwa hiyo hao watu wakateta na Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwani kuteta na mimi? Mbona mnamjaribu BWANA? Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung’unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu?
Kutoka 17:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Jumuiya yote ya Israeli ikaondoka kutoka Jangwa la Sini, ikisafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kama BWANA alivyoagiza. Wakapiga kambi huko Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa. Kwa hiyo wakagombana na Musa wakisema, “Tupe maji ya kunywa.” Musa akajibu, “Mbona mnagombana nami? Kwa nini mnamjaribu BWANA?” Lakini watu walikuwa na kiu huko, wakanungʼunika dhidi ya Musa, wakisema, “Kwa nini ulitutoa kule Misri, ukatuleta hapa utuue kwa kiu sisi, watoto wetu na mifugo yetu?”