Kutoka 15:1-5
Kutoka 15:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Hapo, Mose pamoja na Waisraeli wakamwimbia Mwenyezi-Mungu wimbo huu, “Nitamwimbia Mwenyezi-Mungu kwani ameshinda kwa fahari, farasi na mpandafarasi wake amewatosa baharini. Mwenyezi-Mungu hunijalia nguvu na uwezo, yeye mwenyewe ndiye anayeniokoa. Yeye ni Mungu wangu nami nitamsifu, ni Mungu wa baba yangu nami nitamtukuza. Mwenyezi-Mungu ni shujaa vitani; Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake. “Magari na majeshi ya Farao ameyatumbukiza baharini, maofisa wake wateule wamezama katika bahari ya Shamu. Vilindi vya maji vimewafunika, wameporomoka baharini kama jiwe.
Kutoka 15:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini. BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake. Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini, Maofisa wake wateule wamezama katika Bahari ya Shamu. Vilindi vimewafunikiza, Walizama vilindini kama jiwe.
Kutoka 15:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini. BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake. Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini, Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu. Vilindi vimewafunikiza, Walizama vilindini kama jiwe.
Kutoka 15:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo Musa na Waisraeli wakamwimbia BWANA wimbo huu: “Nitamwimbia BWANA, kwa kuwa ametukuzwa sana. Farasi na mpanda farasi amewatosa baharini. “BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu; amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu, Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. BWANA ni shujaa wa vita; BWANA ndilo jina lake. Magari ya vita ya Farao na jeshi lake amewatosa baharini. Maafisa wa Farao walio bora sana wamezamishwa katika Bahari ya Shamu. Maji yenye kina yamewafunika, wamezama vilindini kama jiwe.