Kutoka 14:13-14
Kutoka 14:13-14 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Musa akawajibu Waisraeli, “Msiogope. Simameni imara, nanyi mtauona wokovu BWANA atakaowapatia leo. Hao Wamisri mnaowaona leo kamwe hamtawaona tena. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mnatakiwa kutulia tu.”
Kutoka 14:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
Kutoka 14:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Mose akawaambia Waisraeli, “Msiogope! Kaeni imara! Leo mtaona jinsi Mwenyezi-Mungu atakavyowaokoa. Maana, hawa Wamisri mnaowaona leo, hamtawaona tena. Mwenyezi-Mungu atawapigania; nyinyi mnachotakiwa kufanya ni kutulia tu.”
Kutoka 14:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
Kutoka 14:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)