Kutoka 11:2-3
Kutoka 11:2-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Waambie Waisraeli sasa wasikie vizuri kwamba kila mmoja wao, mwanamume kwa mwanamke, ni lazima amwombe jirani yake vito vya fedha na dhahabu.” Mwenyezi-Mungu akawafanya Waisraeli wapendeke mbele ya Wamisri. Tena, Mose mwenyewe akawa mtu mashuhuri sana nchini Misri, na mbele ya maofisa wa Farao na watu wote.
Kutoka 11:2-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi nena wewe masikioni mwa watu hawa, na kila mwanamume na atake kwa jirani yake, na kila mwanamke atake kwa jirani yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu. BWANA akawapa watu hao kibali machoni pa Wamisri. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake.
Kutoka 11:2-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi nena wewe masikioni mwa watu hawa, na kila mtu mume na atake kwa jirani yake, na kila mwanamke atake kwa jirani yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu. BWANA akawapa watu hao kibali machoni pa Wamisri. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake.
Kutoka 11:2-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Waambie watu wote kwamba kila mwanaume na kila mwanamke amwombe jirani yake vitu vya fedha na vya dhahabu.” (BWANA akawafanya Wamisri wawe na moyo wa ukarimu kwa Waisraeli, naye Musa mwenyewe akaheshimiwa sana na maafisa wa Farao na watu wote katika nchi ya Misri.)