Kutoka 1:1-8
Kutoka 1:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Haya ndiyo majina ya watoto wa kiume wa Israeli, ambao walikwenda Misri, kila mmoja na jamaa yake: Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zebuluni, Benyamini, Dani, Naftali, Gadi na Asheri. Wazawa wote wa Yakobo walikuwa watu 70. Wakati huo Yosefu alikuwa amekwisha tangulia kukaa huko Misri. Baadaye, Yosefu alifariki, hali kadhalika ndugu zake na kizazi kile chote. Lakini wazawa wa Israeli waliongezeka sana, wakawa wengi na wenye nguvu mno, wakaenea kila mahali nchini Misri. Basi, akatokea mfalme mwingine huko Misri ambaye hakumjua Yosefu.
Kutoka 1:1-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi majina ya wana wa Israeli walioingia Misri ni haya; kila mtu pamoja na jamaa zake walikuja pamoja na Yakobo. Reubeni, na Simeoni na Lawi, na Yuda; na Isakari, na Zabuloni, na Benyamini; na Dani, na Naftali, na Gadi, na Asheri. Na wale watu wote waliotokana na uzao wa Yakobo walikuwa watu sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo. Yusufu akafa, na ndugu zake wote, na watu wote wa kizazi kile. Na wana wa Israeli walikuwa na uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa wengi, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao. Basi akatokea mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.
Kutoka 1:1-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi majina ya wana wa Israeli walioingia Misri ni haya; kila mtu pamoja na jamaa zake walikuja pamoja na Yakobo. Reubeni, na Simeoni na Lawi, na Yuda; na Isakari, na Zabuloni, na Benyamini; na Dani, na Naftali, na Gadi, na Asheri. Na nafsi zile zote zilizotoka viunoni mwa Yakobo zilikuwa ni nafsi sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo. Yusufu akafa, na ndugu zake wote, na watu wote wa kizazi kile. Na wana wa Israeli walikuwa na uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa wengi, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao. Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.
Kutoka 1:1-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli waliokwenda Misri pamoja na Yakobo, kila mmoja na jamaa yake: Reubeni, Simeoni, Lawi na Yuda; Isakari, Zabuloni na Benyamini; Dani na Naftali, Gadi na Asheri. Wazao wote wa Yakobo walikuwa watu sabini; Yusufu alikuwa tayari yuko Misri. Basi Yusufu na kaka zake wote na kizazi kile chote walikufa, lakini Waisraeli walikuwa wamezaana na kuongezeka sana, idadi yao ikawa kubwa mno, hadi wakaijaza nchi. Kisha mfalme mwingine ambaye hakufahamu habari za Yusufu akatawala Misri.