Esta 7:2
Esta 7:2 Biblia Habari Njema (BHN)
Katika siku ya pili, walipokuwa wanakunywa divai, mfalme akamwuliza tena Esta, “Sasa, malkia Esta, unataka nini? Niambie, nawe utapata. Ombi lako ni nini? Hata kama ni nusu ya ufalme wangu, utapewa.”
Shirikisha
Soma Esta 7Esta 7:2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mfalme akamwambia Esta tena siku ya pili pale pale penye karamu ya divai, Malkia Esta, dua yako ni nini? Nawe utapewa; na haja yako ni nini? Hata nusu ya ufalme utatimiziwa.
Shirikisha
Soma Esta 7