Esta 4:8
Esta 4:8 Biblia Habari Njema (BHN)
Alimpa pia nakala moja ya tangazo lililokuwa limetolewa mjini Susa kuhusu kuangamizwa kwa Wayahudi, akamwomba amchukulie Esta, amweleze hali ilivyo, na kumwambia aende kumsihi mfalme na kumwomba awahurumie Wayahudi, watu wake Esta.
Esta 4:8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Pia akampa na nakala ya andiko la mbiu ya kuwaangamiza, iliyotangazwa Shushani, ili amwoneshe Esta, na kumweleza; tena amwagize aingie kwa mfalme, kumsihi na kuwaombea watu wake.
Esta 4:8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Pia akampa na nakili ya andiko la mbiu ya kuwaangamiza, iliyotangazwa Shushani, ili amwonyeshe Esta, na kumweleza; tena amwagize aingie kwa mfalme, kumsihi na kuwaombea watu wake.
Esta 4:8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Akampa nakala ya andiko la amri kwa ajili ya maangamizi yao, lililokuwa limechapishwa huko Shushani, kumwonesha Esta na kumwelezea. Mordekai akamwambia towashi amshawishi Esta kwenda mbele ya mfalme kuomba rehema na kumsihi kwa ajili ya watu wake.