Esta 4:10-12
Esta 4:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Naye Esta akamwambia Hathaki arudi akamwambie Mordekai, “Watumishi wote wa mfalme na raia wa mikoa yote wanajua ya kwamba mtu yeyote yule akiingia katika ua wa ndani na kumwona mfalme bila kuitwa, huyo ni lazima auawe. Anayeweza kunusurika ni yule tu ambaye mfalme atamnyoshea fimbo yake ya dhahabu ili kumsalimisha. Kumbe mimi sijaitwa na mfalme, yapata mwezi mzima sasa.” Mordekai alipopata ujumbe wa Esta
Esta 4:10-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo Esta akasema na Hathaki, akamtuma tena kwa Mordekai, kusema, Watumishi wote wa mfalme wanajua sana, hata na watu wa majimbo ya mfalme, ya kwamba mtu yeyote, akiwa mwanamume au mwanamke, atakayemjia mfalme katika ua wa ndani, wala hakuitwa, kuna sheria moja kwake, ni kwamba auawe; isipokuwa yeye ambaye mfalme atamnyoshea fimbo ya dhahabu, ili aishi; wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku thelathini. Basi wakamwambia Mordekai maneno ya Esta.
Esta 4:10-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo Esta akasema na Hathaki, akamtuma tena kwa Mordekai, kusema, Watumwa wote wa mfalme wanajua sana, hata na watu wa majimbo ya mfalme, ya kwamba mtu ye yote, akiwa mwanamume au mwanamke, atakayemjia mfalme katika ua wa ndani, wala hakuitwa, kuna sheria moja kwake, ni kwamba auawe; isipokuwa yeye ambaye mfalme atamnyoshea fimbo ya dhahabu, ili aishi; wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku thelathini. Basi wakamwambia Mordekai maneno ya Esta.
Esta 4:10-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kisha Esta akamwamuru Hathaki amweleze Mordekai, “Maafisa wote wa mfalme na watu wa majimbo ya ufalme wanajua kuwa mwanaume au mwanamke yeyote ambaye ataingia kumwona mfalme katika ua wa ndani bila kuitwa, mfalme ana sheria moja tu: Atauawa. Njia pekee kinyume na hili ni mfalme kumnyooshea fimbo ya dhahabu ili aishi. Lakini siku thelathini zimepita tangu nilipoitwa kwenda kwa mfalme.” Wakati Mordekai aliarifiwa maneno ya Esta