Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Esta 1:1-9

Esta 1:1-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Hili ndilo lililotokea wakati wa utawala wa Mfalme Ahasuero, yule aliyetawala majimbo mia moja na ishirini na saba (127) kutoka Bara Hindi hadi Kushi. Wakati huo Mfalme Ahasuero alitawala kwenye kiti chake cha ufalme katika ngome ya mji wa Shushani. Katika mwaka wa tatu wa utawala wake, alifanya karamu kwa ajili ya wakuu wake wote pamoja na maafisa. Akawaalika viongozi wa jeshi wa Uajemi na Umedi, wana wa wafalme na wakuu wa majimbo. Kwa muda wa siku mia moja na themanini mfalme alionesha utajiri mwingi wa ufalme wake, fahari na utukufu wa enzi yake. Siku hizo zilipopita, mfalme alifanya karamu kwa muda wa siku saba, katika bustani ya ndani katika jumba la kifalme, kwa ajili ya watu wote kuanzia mdogo hadi mkubwa, waliokuwa katika ngome ya mji wa Shushani. Bustani ilikuwa na mapazia ya kitani nyeupe na buluu, yaliyofungiwa kamba za kitani nyeupe na kitambaa cha zambarau, kwenye pete za fedha juu ya nguzo za marumaru. Kulikuwa na viti vya dhahabu na vya fedha vilivyokuwa vimewekwa kwenye ile sakafu iliyotengenezwa kwa mawe ya rangi, marumaru, lulumizi na mawe mengine ya thamani. Vyombo vya dhahabu vilitumika kwa watu kunywea mvinyo, kila kimoja tofauti na kingine, naye mfalme akatoa mvinyo kwa wingi kwa kadiri ya ukarimu wake. Kwa amri ya mfalme kila mgeni aliruhusiwa kunywa alichotaka, kwa kuwa mfalme alitoa maagizo kwa watumishi wote kugawa mvinyo kila mtu kwa jinsi alivyotaka. Malkia Vashti pia akawafanyia wanawake karamu katika jumba la kifalme la Mfalme Ahasuero.

Shirikisha
Soma Esta 1